Jumuiya kuu ya kanda ya Afrika Magharibi – ECOWAS, imekataa pendekezo la Utawala wa Kijeshi wa Niger la kutaka kufanya uchaguzi ndani ya miaka mitatu, kitu ambacho kinaweza kuzidisha mzozo iwapo kutakuwa hakuna makubaliano yatakayoafikiwa.

ECOWAS na wasuluhishi wengine wenye ushawishi, wamekuwa wakitafuta suluhu za kidiplomasia baada ya mapinduzi ya Kijeshi ya Julai 26 nchini Niger, ambayo ni ya saba katika ukanda wa Afrika Magharibi na Kati, katika kipindi cha miaka mitatu.

Jumuiya hiyo ambayo imekuwa na msimamo mkali zaidi kuhusu Niger kuliko majirani zake wanaoongozwa kijeshi, ilianzisha kikosi cha kikanda ambacho wakuu wa kijeshi wamesema kiko tayari kupelekwa nchini humo iwapo mazungumzo hayatafanikiwa.

Wiki iliyopita, ECOWAS ilisisitiza tena tishio lake la kuingilia kijeshi ikiwa ni siku moja kabla ya serikali ya kijeshi kukubali kukutana na ujumbe wake katika mji mkuu Niamey, na kupelezea nia mpya ya kushirikiana.

Saba kizimbani tuhuma za wizi Bil. 1.23 Katavi
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Agosti 22, 2023