Jeshi la Polisi Mkoani Manyara, kwa kushirikiana na Waandishi wa Habari wamekusudia kushirikiana katika kutoa elimu kwa jamii juu ya kukabiliana na matukio ya kihalifu, ikiwemo ubakaji, Dawa za Kulevya na unyanyasaji wa kijinsia.
Kamanda wa Polisi Mkoani Manyara, George katabazi ameyasema hayo katika mdahalo kuhusu ulinzi na usalama wa Wanahabari ulioandakiwa na Umoja wa Vilabu vya Waandishi Habari Tanzania – UTPC, pamoja na Club ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Manyara – MNRPC.
Amesema, Vyombo vya Habari ni muhimu katika jamii kwa kuwa vinawafikia Wananchi wengi, huku akiahidia kuendelea kushirikiana navyo katika kutekeleza majukumu yao.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi Habari Tanzania – UTPC, Kennedy Simbaya amesema midahalo ya aina hiyo, imekuwa ikifanyika katika Mikoa mbalimbali ikilenga kubaini changamoto za kiusalama zinazowakabili Wanahabari.
Naye mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Manyara, Zacharia Mtigandi amesema Jeshi la Polisi Mkoani Manyara, limekuwa likishirikiana kwa ukaribu na Waandishi wa Habari kwa kutana na changamoto mbalimbali wakati wa utendaji wa kazi zao.