Wizara ya Afya nchini Eritrea imetangaza kuwa hakuna mgonjwa mpya wa Corona nchi humo baada ya mgonjwa wa 39 ambaye ndiye mgonjwa wa mwisho nchini humo kuruhusiwa kutoka Hospitali.

Taarifa ya wizara imesema mgonjwa mmoja amepona baada ya vipimo kuonesha hana maambukizi na ameruhusiwa kutoka hospitali, majibu haya yanaashiria kuwa Wagonjwa wote 39 wamepona.

Hata hivyo wizara imewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari za kujikinga na ugonjwa huo kama Wataalam wanavyoeleza hadi hapo Kikosi Kazi kitakapofanya uchunguzi na kujiridhisha kuwa hakuna kabisa  virusi vya Corona Eritrea.

Nchi hiyo ni miongoni mwa nchi chache za Africa ambazo zilikuwa hazijatangaza kifo cha Covid 19 hadi kufikia jana, nyingine ni Madagascar, Afrika ya Kati, Msumbiji, Namibia, Seychelles, Lesotho, Rwanda na Uganda.

Simba SC kumsajili Mukoko Tonombe?
Mchezaji wa Arsenal yu mahututi