Mabingwa wa soka Tanzania bara Wekundu Wa Msimbazi Simba wanatajwa kuwa kwenye mipango mizuri ya kumsajili kiungo wa timu ya Taifa ya DR Congo na klabu ya AS Vita, Mukoko Tonombe.

Tonombe ambaye mkataba wake upo mbioni kumalizika katika klabu hiyo, atakuwa mchezaji huru mwishoni mwa msimu huu, na Simba imekua klabu pakee ya Tanzania inayotajwa kuwa kwenye harakati za kumsajili.

Kiungo huyo mwenye umri Wa miaka 24, amekuwa katika kiwango bora na kutoa mchango mkubwa kwenye kikosi cha AS vita kilichotinga hatua ya makundi michuano ya klabu bingwa barani Afrika msimu huu.

Hata hivyo mtendaji mkuu wa klabu ya Simba Senzo Mazinginza aliwataka mashabiki na wanachama kuwa wastahamioivu katika kipindi hiki ambacho wanaendelea kuyafanyia kazi maombi na mapendekezo ya benchi la ufundi.

Kiongozi huyo alisema wanatambua wanachama na mashabiki wana hamu ya kuona kiosi chao kinakua bora kwa msimu ujao wa ligi kuu na michuano ya kimataifa, hivyo amewasisitiza kuwa watulivu na kuwaachia kazi viongozi wao.

Muuza duka afariki kwa ajali ya moto dukani
Eritrea : wagonjwa wote wa Covid -19 wamepona