Nandy, ni jina jipya la msanii wa kike linaloipeperusha bendera ya Tanzania kimuziki barani Afrika kuibuka mshindi wa pili wa shindano kubwa la Tecno Own The Stage, ambalo lilikuwa shindano la kwanza la Kareoke barani Afrika.

Hata hivyo, kwa Tanzania sio jina jipya kwani ni msanii aliyefanya kazi nyingi na kushirikiana na wasanii wengi wakubwa, akikoreza kiitikio cha ‘Kabinti’ ya Dully Sykes.

Nandy

February 7 mwaka huu, Nandy alitajwa kuwa mshindi wa pili wa shindano hilo akimfuatia mshindi wa kwanza ambaye ni raia wa Nigeria, Shapeera.

Nandy alikabidhiwa kitita cha $15,000 ambazo ni sawa na zaidi ya shilingi milioni 36 za Tanzania pamoja na kupewa nafasi adhibu ya kujiunga na label ya Chocolate City ya Nigeria akijiunga na wasanii wakubwa kama Victoria Kimani, M.I na Ice Prince.

Dar24 imefanya mahojiano maalum na Nandy, msikilize hapa:

Ray C alia na Ukata, aeleza mtindo anaotumia kupanda daladala bila kutambulika
Juventus Vs Bayern Munich, Guardiola Asaka Namna Ya Kuondoka Kwa Heshima