Chama cha soka nchini England FA, kimeonyesha kuchukizwa na maamuzi yaliyochukuliwa na meneja wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho dhidi ya daktari wa kikosi chake Eva Carneiro wakati wa mchezo wa ufunguzi wa ligi ya nchini humo msimu wa 2015-16.

Mtendaji mkuu wa chama cha soka nchini humo FA, Martin Glenn amesema wameshangazwa na adhabu ya daktari huyo kuendelea kuchukua nafasi kwa kigezo cha kuwajibishwa na mkuu wa benchi la ufundi la Chelsea.

Glenn amesema jambo hilo linawasikitisha lakini wanashindwa kuingilia kati kutokana na mazingira ya kesi hiyo kutowahusu kwa asilimi kubwa hasa ikizingatiwa daktari Eva yupo chini ya mkuu wa benhi la ufundi.

Amesema wamekua wakifuatilia picha za televisheni za tukio lililosababisha Eva kutofautiana na bosi wake mara kwa mara, lakini mpaka sasa hawajaona kosa lolote ambalo lilisababisha uamuzi wa kuwekwa pembeni kuchukuliwa na Jose Mourinho.

Hata hivyo Glenn alilizungumzia jambo hilo akiwa kwenye mkutano wa Soccerex Football Business uliofanyika mjini Manchester, baada ya kuulizwa na waandishi wa habari nini hatua ya FA juu ya tukio hilo ambalo limeonyesha kutokua na haki kwa mwanadada Eva.

Eva Carneiro, alipigwa stop ya kukaa kwenye benchi pamoja na kufika kwenye kambi ya kikosi cha Chelsea kwa ajili ya kufanya kazi yake na tayari wasaidizi wake wameshateuliwa kuendelea kufanya majukumu ya kuwapa huduma za kitabibu wachezaji.

Lakini pamoja na yote hayo kutokea Eva Carneiro, bado anaendelea kuwa mkuu wa kitengo cha matabibu wa klabu ya Chelsea.

Ray C: Najua Mpango Wao Ni Kuniua
Azam Media Wadhamini Kombe La Shirikisho