Miamba ya Soka nchini Misri Al Ahly imeendelea kutajwa kuwa kwenye mpango wa kumsajili Mshambuliaji na Nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Mbwana Ally Samatta.

Samatta kwa sasa yupo nchini Ubelgiji akicheza kwa mkopo kwenye klabu ya KRC Genk, akitokea Fenerbahce baada ya kukosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Kocha Jorge Jesus.

Al Ahly inayoshikilia Rekodi ya kutwaa Ubingwa wa Afrika mara nyingi, imeendelea kubaki kwenye dili hilo kufuatia kukwama katika usajili wa Mshambuliaji kutoka DR Congo Jackson Muleka.

Mpango wa usajili wa Muleka umekwama kutokana na Klabu ya Besiktas anayoichezea kutaka kiwango kikubwa zaidi cha fedha.

Hata hivyo Al Ahly wamedhamiria kumsajili Samatta kwa mkopo katika kipindi hiki cha usajili wa Dirisha Dogo, huku thamani ya Mshambuliaji huyo ikitajwa kufikia Dola za Marekani Milioni 2.7.

Kwa mujibu wa ripoti ya Sporx, Fenerbahce wanataka kumpiga bei Samatta katika dirisha hili la usajili kufuatia kocha wao Jorge Jesus, kuendelea na msimamo wa kutomuhitaji katika mipango yake.

Inaelezwa Al Ahly inataka kukamilisha usajili wa Mshambuliaji wa kati kabla ya Kombe la Dunia la Klabu la FIFA mwezi ujao.

Shambulio kijijini lauwa 15, wengi ni Wanawake na Watoto
Shirika la KLM laiomba radhi Tanzania