Gwiji wa klabu ya Everton, Duncan Ferguson amempongeza na kumshukuru mshambuliaji na nahodha wa klabu ya Man Utd, Wayne Mark Rooney kwa kukubali kurejea Goodson Park baada ya miaka 11.

Rooney, alionekana kwa mara ya kwanza akiwa amevaa jezi za klabu ya Everton ambayo ilimkuza na kisha kumuuza kwenye klabu ya Man Utd kwa ada ya usajili wa paund million 27 mnamo mwaka 2004.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 29, alirejea klabuni hapo kufuatia mualiko alioupokea kutoka kwa Duncan Ferguson ambaye aliwahi kucheza naye huko Goodson Park.

Rooney, alijumuika na wachezaji wa Everton katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Villareal ambapo kila shabiki wa The Toffees alionekana akifurahia kitendo cha mshambuliaji huo kurejea nyumbani.

Katika mchezo huo Rooney alivalia jezi yenye namba 18, na alikua akifuata maelekezo yote ya meneja wa klabu ya Everton, Roberto Martinez.

Naye Duncan Ferguson alijumuika na wachezaji wengine wa Everton katika mchezo huo ambao ulimalizika kwa wenyeji kupata ushindi wa mabao mawili kwa moja dhidi ya wageni kutoka nchini Hispania Villareal.

Jeshi La Nigeria Lawakalia Kooni Boko Haram, Kiongozi Wao Atoweka
Zitto Kabwe: Lowassa Na Magufuli Hawauwezi Ufisadi