Klabu ya Chelsea inajipanga kumpa nafasi Frank Lampard ya kurejea klabuni hapo, baada ya kuthibitika ataondoka New York City FC kufuatia mkataba wake kufikia kikomo.

Lampard mwenye umri wa miaka 38, ametangaza kuachia ngazi baada ya kukutana na viongozi wa klabu ya New York City FC, na kuelezwa kuhusu suala la kutosaini mkataba mpya.

Uongozi wa klabu ya Chelsea unaamini kiungo huyo ambaye aliitumikia The Blues kwa miaka 13 ataitikia wito wa kurejea klabuni hapo.

Kazi kubwa ambayo Chelsea wamemuandalia Lampard ni kuwa sehemu ya benchi la ufundi klabuni hapo, ambapo kwa kiasi kikubwa atatumika kama mtu wa kuleta hamasa kwa wachezaji.

Hata hivyo mpaka sasa  Lampard hajaonyesha dhamira ya kuwa tayari kurejea Stamford Bridge, kufuatia ukimya uliotawala, na tangu alipoanza kuhojiwa kuhusu mustakabali wake mara atakapoondoka nchini Marekani hajaizungumza Chelsea.

Video: 'Sheria ya mirathi iliyopo ni ya kibaguzi na kandamizi' - WLAC
CCM yatuhumiwa kuuza shule kinyemela, yadai elimu bure imechangia