Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake na Watoto (WLAC)  kimetoa wito kwa Serikali kutoa kipaumbele katika suala la marekebisho ya sheria za mirathi ya kimila kwani sheria iliyopo ni ya kibaguzi na kandamizi kwa wanawake na watoto wa kike.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho, Theodosia Muhulo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo Ofisini kwake Jijini Dar es salaam, Muhulo amesema sheria hiyo inakinzana  na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kama ilivyofanyiwa  mabadiliko.

Aidha, ameiomba Serikali kutekeleza mkataba wa Kuondoa Aina zote za Ubaguzi dhidi ya Wanawake  (CEDAW) kwa kuufanya kuwa sehemu ya sheria za nchi na kuondoa aina zote za ubaguzi dhidi ya wanawake na kutoa elimu kwa jamii ili kuondokanakana na mila potofu dhidi ya wanawake na watoto wa kike.

Hata hivyo amesema kuwa WLAC imefanya shughuli mbambali za kisheria  kwa kushirikiana na  na wadau wa haki za binadamu, ikiwemo kuelimisha jamii kuhusu sheria zinazohusu masuala ya wanawake na watoto wa kike.

Muhulo, ameongeza kuwa  elimu kuhusu sheria za mirathi  na uwepo wa mikataba mbalimbali ya kikanda na kimataifa, kama mkataba wa kuondoa aina zote za ubaguzi dhidi ya wanawake (CEDAW) ambayo nchi imeridhia na namna ya kudai haki za wanawake itasaidia kuondoa tatizo hili.

 

Video: Wajane wakimbilia Dar kutafuta maisha
Frank Lampard Kurejea Stamford Bridge