Kocha Christophe Galtier amefukuzwa Paris Saint-Germain baada ya kushinda taji la Ligi Kuu Ufaransa, Ligue 1, vyanzo vimeiambia ESPN.

Galtier aliiongoza PSG kutwaa taji la ligi hiyo kwa msimu wa 2022/23 lakini akashindwa kuleta mafanikio kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, huku klabu hiyo ya Ufaransa ikitolewa na Bay- ern Munich katika hatua ya 16 bora.

Kwa mujibu wa vyanzo vya ESPN, Mkurugenzi wa Michezo wa PSG, Luis Campos, alifahamisha Galtier alifukuzwa na klabu hiyo Jumanne huku kocha zamani wa Bayern Munich, Julian Nagelsmann, akiendelea na mazungumzo na klabu hiyo.

Vyanzo vya habari viliongeza klabu hiyo pia ilifanya mazungumzo na kocha wa zamani wa Timu ya Taifa ya Hispania na Barcelona, Luis Enrique, lakini sasa wamemfanya Nagelsmann kuwa mlengwa wao mkuu, huku kocha huyo wa Ujerumani akitamani, Thierry Henry ajiunge naye kama msaidizi wake.

Kuna imani inayoongezeka makubaliano yanaweza kufanywa kwa Nagelsmann na Henry kujiunga na mabingwa hao wa Ufaransa.

Galtier alijiunga na PSG msimu uliopita wa joto baada ya kuiongoza Nice kumaliza katika nafasi ya tisa msimu wa 2021-22 na amekuwa na majukumu ya kuinoa Lille na Saint- Etienne.

Lionel Messi na Sergio Ramos pia wataondoka katika klabu hiyo msimu huu wa joto baada ya kumalizika kwa mikataba yao.

Vyanzo viliiambia ESPN mnamo Mei, mwaka huu Neymar pia yuko tayari kuondoka PSG msimu wa joto na klabu iko tayari kumwachia ikiwa watapata ofa inayofaa.

Tano Ligi Kuu hatarini kucheza Play Off
Rasmi Feisal Salum aondoka Young Africans