Mlinda mlango kutoka nchini Italia na klabu ya Juventus, Gianluigi Boffon ameelezea kufurahishwa na umakini wa safu yake ya ulinzi katika mchezo wa seria A dhidi ya SSC Napoli.

Katika mchezo huo uliochezwa mwishoni mwa juma lililopita, Juve iliibuka na ushindi wa bao moja kwa sifuri na kuifanya klabu hiyo inayonolewa na meneja Massimiliano Allegro,  kucheza michezo minane bila kufungwa.

Mkongwe huyo aliwataja Andrea Barzagli, Leonardo Bonucci na Giorgio Chiellini kama mabeki muhimu walioisaidia Juve kuzoa pointi zote tatu dhidi ya vinara hao.

“Zikiwa zimebaki dakika 25, tulitakiwa kukazana. Sare isingekuwa mbaya, lakini nilihisi kuchukua pointi tatu ni muhimu zaidi. ”

“Bado kuna mechi 13 zilizobaki na tuna nafasi ya kurekebisha hali ya mambo kwa kipindi cha msimu kilichobaki,” alisema.

Guus Hiddink Aichana Ligi Ya Ufaransa
Simba Yaendelea Kuneemeka Na Usajili Wa Kimataifa