Meneja wa klabu bingwa nchini Uingereza, Chelsea FC, Guus Hiddink ameiponda Ligi ya Ufaransa, Ligue 1 kwa kusema haina ushindani wa kutosha kwa wachezaji wenye uwezo kama wa Eden Hazard.

Hiddink amejikuta akiizungumza suala la ligi ya nchini Ufaransa, kufuatia mchezaji wake Eden Hazard kuhusishwa na mipango ya kutaka kujiunga na mabingwa wa soka nchini humo Paris Saint-Germain.

Kiungo huyo mshambuliaji kutoka nchini Ubelgiji ambaye alijiunga na Blues akitokea kwenye klabu ya Lille ya nchini Ufaransa, hivi karibuni alikaririwa akisema kwamba inaweza kuwa vigumu kukataa ofa kutoka PSG.

Hata hivyo,  pamoja na klabu ya PSG kuanza kuonekana kuwa tishio barani Ulaya, Hiddink amesema wachezaji wenye uwezo hawawezi kutaka kucheza kwenye Ligi isiyokuwa na ushindani.

“PSG wana nia kubwa ya kutaka kutwaa ubingwa wa Klabu Bingwa Ulaya,” alisema Hiddink katika mkutano wake na waandishi wa habari.

“Hatua kwa hatua wamekuwa wakionyesha nia yao ya kutaka kuwa timu kubwa Ukawa. Hivyo,  ushindani huo naweza kuufahamu lakini Ligi yao ni tofauti na kwa sasa naweza kusema wapo kileleni kwa tofauti ya pointi 24,” aliongeza kocha huyo.

Amesema anachoamini ni kwamba wachezji bora huwa wanapenda kucheza kwenye ligi zenye ushindani kama ligi kuu ya soka ya Uingereza, La Liga ama Bundesliga.

Ligi Kuu Mzunguko Wa 20 Wikiendi Hii
Gianluigi Boffon Afurahishwa Na Ukuta Wa Juventus