Benchi la Ufundi la Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC, limefanya kikao na wachezaji wote wa klabu hiyo, baada ya kucheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya FAR Rabat mwishoni mwa juma lililopita.

Simba SC ililazimisha sare ya 2-2, kwenye mchezo huo ambao ulikuwa wa kwanza tangu Mabingwa hao wa Tanzania Bara walipoanza kambi nchini Morocco majuma mawili yaliyopita.

Kocha Mkuu Didier Gomes amesema lengo kuu la kikao hicho ni kuwaweka sawa wachezaji wake wote ambao wapo kambini kwa sasa, hasa baada ya kuona mazuri na mapungufu kwenye mchezo dhidi ya FAR Rabat.

Kocha huyo amesema: “Wachezaji wapya hawaifahamu vema falsafa ya Simba na kuielewa kiundani timu yao, hivyo baada ya mechi tulikuwa na kikao nao maalumu kuwaeleza kwa kina kuhusu timu hii na mipango yake kabla ya kutafuta mechi nyingine za kirafiki kuendelea kuwasoma vizuri wachezaji wangu,”

“Ni mechi muhimu kwetu kila mmoja kupima kiwango chake, lakini pia itatusaidia kuona nini tunapaswa kurekebisha kwenye kikosi chetu, ila mpaka sasa vijana wangu wanazidi kuimarika, na hasa baada ya wachezaji wapya kujumuika pamoja na wenzao.”

Katika hatau nyingine imefahamika kuwa Simba SC itacheza mchezo mingine miwili ya kirafiki, kabla ya kurejea nchini mwanzoni mwa ujao.

Udahili shahada ya kwanza katika taasisi za elimu ya juu kuanza Agosti 24
Mbowe afikishwa Mahakamani kwa hati ya Dharula