Muamuzi mstaafu kutoka nchini England, Graham Poll, amesema kulikua hakuna sababu kwa muamuzi kutoka nchini Italia, Nicola Rizzoli kushindwa kumuadhibu beki Hector Moreno, baada ya kumchezea hovyo beki wa pembeni wa Man Utd,  Luke Shaw wakati wa mchezo wa ufunguzi hatua ya makundu uliochezwa usiku wa kuamkia jana.

Graham Poll aliyetangaza kustaafu uamuzi mwaka 2007, amesema muamuzi Nicola Rizzoli alishindwa kutimiza wajibu wake kwa kumpa adhabu beki wa PSV Eindhoven ambaye alionekana akifanya kosa kwa makusudi.

Poll amesema haamini kama Moreno alifanya tukio la kumuangusha Shaw kwa bahati mbaya, kutokana na uhalisia wa mazingira ya wawili hao yalivyokua hivyo anaamini muamuzi Rozzoli alichemka.

                                                  Graham Poll wakati akiwa kazini kabl ya kutangaza kustaafu mwaka 2007

Amesema alishangazwa na muamuzi huyo kushindwa hata kuwapa penati Man Utd kutokana na tukio la kuangushwa kwa Shaw kwenye eneo la hatari, na badala yake aliamuru mpira wa kona kupigwa kuelekea lango la PSV.

Hata hivyo muamuzi huyo mstaafu ametoa angalizo kwa vyombo vya habari kutomchukulia kama anawatetea Man utd kwa maslahi ya nchi yake ya England, bali amelazimika kuzungumza jambo hilo kutokana na taaluma na uweledi wa muamuzi anayepewa jukumu la kuchezesha michezo ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Magufuli Ajivisha Joho La Kampeni Ya Chadema
Pacquiao: Akirudi Poa, Asiporudi Poa