Mshambuliaji Habib Kyombo amekua mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Singida Big Stars itakayoshiriki kwa mara ya kwanza Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao 2022/23.

Kyombo anayemalizia mkataba wake Mbeya Kwanza FC, amekamilisha dili la kujiunga na klabu hiyo, leo Jumanne (Juni 21) mchana, kisha kuthibitishwa kupitia katika Kurasa za Mitandao ya Kijamii za Singida Big Stars.

Mchezaji huyo ambaye alibahatika kusajiliwa Mamelodi Sondowns ya Afrika Kusini, alihusishwa kujiunga na Simba SC mwishoni mwa juma lililopita, hivyo kusajiliwa Singida Bid Stars kunasitisha tetesi hizo.  

Taarifa za Singida Big Stars za kuthibitisha kumsajili Mshambuliaji huyo zilizotolewa kwenye ukurasa wa Instagram wa klabu hiyo zimeeleza:

RASMI: Habib Kyombo ni BIG STAR ⭐️

Karibu fundi wa mpira uitumikie klabu yako pendwa katika msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier League 2022/2023).

Polisi 'yadaka' mzigo wa mirungi ukisafirishwa
Ukraine yazidi kujiuliza kwa Urusi