Chama Cha Demokrasia na Maendeleo kimewataka Wabunge Wanawake 19 walioapishwa jana akiwemo Halima Mdee na Ester Bulaya kufika Makao Makuu ya chama Novemba 27, Ijumaa kujieleza baada ya kuapishwa bila ridhaa ya chama hicho.

Akizungumza na vyombo vya habari leo Novemba 25 jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa chama hicho , John Mnyika amesema Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe ataongoza kuwahoji.

“Naomba kutangaza Wito (Public Notice) kwa Wanachama wetu 19 waliokula kiapo jana Bungeni dodoma kufika katika ofisi za Makao Makuu ya Chama Dar es Salaam siku ya Ijumaa tarehe 27 Novemba 2020 saa 2 asubuhi,” amesema Mnyika.

CHADEMA yawakana mdee na wenzie

Aidha Mnyika amesema kuwa hii si mara ya kwanza kwa chama hicho kufanya vikao vya kinidhamu.

Ngorongoro Heroes kuikabili Somalia
Mo Dewji, Kigwangala mambo safi

Comments

comments