Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba SC Zakaria Hanspope amesema waamuzi ni tatizo kubwa kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara, anaamini kama wangekuwa wanachezesha kwa haki, wasingefungwa na Young Africans July 3, kwani walinyimwa penati zao mbili.

Hans Pope ameshauri ili kuondoa utata kwenye maamuzi ya marefa, inabidi (VAR) ‘Video Assistant Referees’ itumike kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara.

Pia kuhusu klabu ya Simba kutwaa ubingwa wa Ligi mara nne mfululizo, amesema ; “Sijaona progress ya vilabu vingine vyote kwenye ligi kuu Tanzania bara, na iwapo havitojizatiti, Simba sc itaendelea kutwaa ubingwa na kutawala kwa misimu mingi mingine ijayo.

“Hadi sasa nina maombi ya Wachezaji (11) wakimataifa wanaotaka nafasi Simba SC”

“Kwa sasa Wachezaji wengi wanatamani kuja Simba SC, nakuhakikishia hakuna Mchezaji tutakayemuhitaji wa nje tukimtaka tutamkosa, labda wa hapa nyumbani”

“Kuhusu kwamba tumemleta Jean Makusu halafu watani zetu Young Africans wametupora, mimi sijui, kama kuja watakuwa wamekuja wenyewe, sisi hatujaleta mtu, Sisi tunasajiri hatushindani na mtu”
amesema Hasnpope

Simba Queens kukabidhiwa taji la Ligi Kuu leo
Mwigulu: Young Africans itakuwa imara 2021-22