Aliyekua kocha mkuu wa timu ya taifa ya Misri, Hassan Shehata ameombwa kuchukua nafasi ya Alex Mcleish Zamalek.

Mcleish amejikuta katika wakati mgumu siku za karibuni mbele ya Mwenyekiti wa Zamalek, Mortada Mansour kutokana na timu kucheza vibaya mechi zake.

Mansour pia amewafukuza Wasaidizi wa Mcleish na kuwateua Mohamed Helmy na Gamal Abdel-Hameed.

McLeish baada ya kutibuana na Mansour ambaye pia alimfukuza Frank Nuttal, amempa kocha huyo wa zamani wa Aston Villa saa 24 kuamua kubaki au kuondoka.

Baada ya kuachana Arab Contractors, Hassan Shehata aliweka wazi anaweza kujiunga na Zamalek na muda wote huo hakuwa na kazi ingawa tetesi zilikuwa zinasema antakiwa na timu ya taifa ya Syria.

Pia amemuomba daktari Mkuu wa zamani wa timu hiyo, Dk. Ayman Farid kurejea kazini.

Mara ya mwisho Dk. Farid alikuwa na kocha Mreno, Jesualdo Ferreira, timu hiyo ikitwaa ubingwa wa Misri na Kombe. Pia amefanya kazi na Shehata alipokuwa kwenye timu hiyo mwaka 2011.

CAG, Msajili wa Hazina wakinzana kuhusu Umiliki wa PRIDE
MAPENDEKEZO YA SHERIA YA WAZEE YATUA BUNGENI