Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Beno Malisa  amezitaka mamlaka husika kuwachukulia hatua viongozi na wote watakaojihusisha na uharibifu wa Misitu na vyanzo vya maji Mkoani Mbeya.

Malisa ameyasema hayo mara baada ya kuhitimisha zoezi la upandaji wa Miti katika eneo la shule katika Kijiji cha Iwala Halmashauri ya Wilaya Mbeya.

Agizo hilo ambalo alilitoa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, Malisa amewasisitiza Wakurugenzi na Madiwani Mkoani Mbeya kwenda kusimamia Sheria zilizopo za uhifadhi wa Misitu na Mazingira ili kukomesha vitendo vya uvamizi katika Maeneo hayo tengefu.

Amesema, “kwa Mkoa wa Mbeya umeweka malengo kwa kila Halmashauri Mkoani humo kupanda miti Milioni 1.5 na kuisimamia ili kufanya tathmini ya miti iliyopandwa.”

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Mbeya,  Stephen  Katemba amesema Halmashauri itaendelea kupanda zaidi Miti hii itasaidia kutunz Mazingira na kuingiza kipato kinachotokana na Miti hiyo ambapo takribani Milioni 420 imekusanya kutokana na Mazao yatokanayo na Miti hii ni kwa kushirikiana na Tfs

Naye Meneja wa TFS Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Cosmas Ndakidemi Amesema kwa Mwaka huu Miti itatolewa hivyo wito kwa Wananchi wa Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini Kujitokeza kuchukua Miche na Kupanda kwa kipindi hiki cha Mvua

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Februari 6, 2024
Vijiji nane Ngorongoro kunufaika Mradi wa Maji Mageri