Bila shaka utakuwa umewahi kulisikia neno Katerero ambalo limepata umaarufu mkubwa hapa nchini, lakini tafsiri ya wengi huwa ni tofauti na maana halisi ya neno hilo.
Dar24 Media imeamua kufuatilia ukweli na kufika moja kwa moja katika eneo hilo la Katerero, ili kupata historia ya jina Katerero na jinsi lilivyopatikana.
Kwa nyakati tofauti tofauti, wakazi wa eneo hilo wanasema neno Katerero limetokana na enzi za Masultani kutumia sehemu ya mlima unaopatikana hapo ambapo kuna uwanja uliotumika kuwaadhibu watu wanaofanya makosa.
Aidha, wamesema eneo hilo pia lina Mlima uliotumika kama wa uwanja wa mapambano enzi za Wakoloni na baadaye likawepo Gulio maarufu lililotumika na wafanyabiashara.