Katika hali isiyo ya kawaida, Hospitali moja imebainika kuwashawishi wanawake wajawazito waliokuwa na mpango wa kutoa mimba, kutunza ujauzitio huo ili waweze kuwauza watoto hao kwa watu wanaohitaji na kuwalipa kiasi cha fedha.

Hospitali hiyo iliyotajwa kwa jina la Palash iliyoko katika wilaya ya Gwailor nchini India, imekuwa ikiwauza vichanga kwa wenye ndoa walioshindwa kupata watoto na wanahitaji kupata, kwa kiasi cha $1,400 (Sawa na shilingili 3,055,010 za Tanzania) kwa kila mtoto mchanga.

Afisa wa Polisi kutoka katika kitengo cha makosa ya jinai alilimbia gazeti la ‘Times of India’ kuwa wamebaini tayari hospitali hiyo ilishawauza watoto wachanga watano.

Alisema kuwa watatu kati ya hao tayari wameshajulikana walikonunuliwa na watu waliowanunua lakini wawili hawajapatikana hadi sasa.

Meneja wa Hospitali hiyo, Arun Bhadoria ambaye alikamatwa na Jeshi la Polisi nchini humo, alieleza kuwa hospitali hiyo ilikuwa ikifanya juhudi za kuwatafuta mtaani wasichana waliopata ujauzito wasiotaka na kuwashawishi kuutunza kwa malipo ili wawaachie watoto.

Kabwe ahoji kulipwa fidia baada ya uchunguzi wa kutumbuliwa jipu
Yanga yajipanga kuumana na Al Ahly, Mtihani wenye majibu yaliyojificha