Baada ya kusafiri mpaka nchini Uganda na Djibouti mwaka  huu  mahakama ya uhalifu wa kivita Imeijia juu nchi hizo mbili kwa kushindwa kumkamata Rais wa Sudan Omar al Bashir.

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC imesema itazishitaki serikali za Uganda na Djibouti kwa baraza la usalama la umoja wa mataifa kwa kushindwa kumtia nguvuni Rais wa Sudan Omar al Bashir alipozuru katika nchi zao.

Bashir anatuhumiwa kwa mauaji ya kimbari,uhalifu dhidi ya binaadam pamoja na kusababisha vita katika jimbo la Darfur pamoja na kuwa amekuwa akikana mashikata hayo.

Mahakama hiyo ICC imesema kuwa nchi hizo mbili zilipaswa kumtia nguvuni Bashir kwakuwa zilisaini mkataba na mahakama hiyo.

Picha: Roma, Kala Jeremiah wamtembelea Lowassa
Shilole Arudi Darasani kwa Ajili ya Lugha