Kikosi cha Man City kimeendelea kupata pigo, baada ya kuwapoteza wachezaji wake wengine wawili katika michezo ya juma lililopita.

Man City wamempoteza Joe Hart na Raheem Sterling baada ya kuumia wakati wa mchezo wa jana wa ligi kuu ya soka nchini England, hali ambayo inaendelea kuzidisha hofu kwa meneja Manuel Pellegrini.

Wawili hao pia wameigharimu timu ya taifa ya England, ambayo juma hili itakabiliwa na michezo miwili ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Ujerumani pamoja na Uholanzi.

Hart aliumia mguu wake wa kulia, akiwa katika harakati za kumuwahi mshambuliaji wa Man Utd, Anthony Martial, alipokua katika harakati za kulisabahi lango lake baada ya beki Martin Demichelis kurudisha mpira kwa pasi mkaa.

Hart was caught short by a poor Demichelis back pass and the England goalkeeper had to slide in to stop Anthony MartialKipa wa Manchester City Joe Hart katika tukio lililomletea majanga

Sterling went off in the first half after suffering the injury following a tackle from Juan Mata (right)Sterling aliumia baada ya kuvaana na Juan Mata

Sterling naye alitolewa nje ya uwanja katika kipindi cha kwanza baada ya kugongana na Juan Mata.

Kwa mujibu wa meneja wa Man City, Manuel Pellegrini wachezaji hao huenda wakawa nje ya uwanja kwa kipindi cha mwezi mmoja, hatua ambayo inadhihirisha kikosi cha matajiri hao wa jijini Manchester wanaendelea kupungukiwa wachezaji wake muhimu siku hadi siku.

Katikati ya juma lililopita, Man City walimpoteza beki wao wa kati Vincent Kompany, pamoja na Nicolás Otamendi baada ya kuumia wakati wa mchezo wa hatua ya 16 bora wa ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Azam FC Kupambana Na Esperance Sportive de Tunis
Remi Garde Kufungasha Na Kurejea Nyumbani Ufaransa