Mwanamuziki maarufu nchini Marekani Shawn Corey Carter maarufu Jay-Z amemfikisha Mahakamani mpiga picha wake wa zamani Jonathan Mannion pamoja na kampuni yake kwa kuuza baadhi ya picha zake.
Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ Jay-Z amesema kuwa Mannion ameuza baadhi ya picha zake bila rusa yake ambapo baadhi ameziuza kwa maelfu ya dola za Kimarekani.
Msanii huyo amesema kuwa ameshangazwa na mpiga picha Mannion kuuza picha ambazo walipiga kwaajili kuzitumia kwenye cover ya album yake, Reasonable Doubt ambazo hazikutumika kwenye kazi hiyo .
Kwenye shtaka lake Jay-Z amesema huu ni utumiaji mbaya wa jina lake pamoja na picha.
Ameeleza kuwa kila alipokuwa akimuomba kuacha kutumia vibaya picha zake, mpiga picha huyo alihitaji kiasi cha fedha takribani Dola Milioni 10 za Kimarekani.