Dunia ina mambo na huenda yasiishe hadi siku moja itakaposimama na kuwashusha binadamu wote ibaki tupu! Hivi ndivyo unavyoweza kusema katika hukumu iliyosomwa wiki iliyopita dhidi ya mwanaume mmoja aliyeoa mama na mwanae.
Mahakama ya Pennsylvania nchini Marekani imemhukumu kifungo cha miaka miwili jela, Christopher Hauptmann kwa kosa la kumuoa mwanamke mwenye umri wa miaka 43 pamoja na binti yake mwenye umri wa miaka 18.
Hauptmann mwenye umri wa miaka 44, amethibitika kuwa alitumia nyaraka za uongo kuidanganya Serikali ili aweze kufunga ndoa na binti huyo wa mkewe.
Ushahidi uliowasilishwa mahakamani hapo umeeleza kuwa Hauptmann alifunga ndoa mwaka 2015 na Shannon Deitrich, lakini mwaka uliofuata alibadili jina lake kwa kughushi kuwa anaitwa Christopher Buckley na kupata kibali cha kufunga ndoa nyingine na Kaylee Durovick ambaye ni binti wa mkewe huyo wa kwanza.
- Wingi wa wanafunzi kidato cha kwanza kupelekea kuanzishwa shule mpya.
- Video: Tundu Lissu achambuliwa, NEC yazijibu hoja za Ukawa
Mama Deitrich alitoa ushahidi uliopelekea kumtia hatiani mwanaume huyo kwani mbali na mambo mengine hakuwahi kumpa talaka.
Mahakama imeamuru mwanaume huyo asimsogelee tena Deitrich, lakini taarifa zinasema bado ameendelea kuwa mume wa binti yake.