Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Young Africans, Jerry Muro amesema mwenye uwezo wa kumwambia asijihusishe na masuala ya soka ni mwajiri wake ambaye ni Klabu ya Young Africans na siyo mtu mwingine.

Muro ametangaza suala hilo baada ya Kamati ya Maadili ya Shirikisho la soka nchini TFF kutangaza kumfungia kutojihusisha na masuala ya soka kwa kipindi cha mwaka mmoja sambamba na kumtaka alipe faini ya shilingi milioni tatu (3,000,000), kwa kile kinachodaiwa ni kupingana na maagizo ya TFF.

“TFF haina uwezo wa kunifungia, kwani mimi ni mwanachama ama muajiri wao?,

“Mimi nitakua radhi kunyamaza pale nitakapo takiwa kufanya hivyo na uongozi wa Young Africans ambao ndio umeniajiuri kufanya kazi ya usemaji” Alisema Muro alipozungumza na Dar24.com

Jerry Muro aliingia kwenye matatizo na TFF, baada ya kuzungumza na vyombo vya habari siku chache kabla ya mchezo wa hatua ya robo fainali ya kombe la shirikisho dhidi ya TP Mazembe uliochwezwa nchini mwishoni mwa mwezi uliopita, ambapo alipinga agizo la ukaaji wa mashabiki wa soka katika uwanja wa taifa kwa kuzingatia itikazi za Usimba na Uyanga.

Juventus FC Wafanya Kweli Kwa Alexis Sanchez
Video: Mauaji Dallas, Marekani