Baada ya kufanya usajili wa mlinda mlango pekee wakati wa majira ya kiangazi, meneja wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger anapewa nafasi kubwa ya kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid, Jese Rodriguez itakapofika mwezi januari mwaka 2016.

Mshambuliaji huyo yupo kwenye mikakati ya kutaka kuondoka Real Madrid kutokana na ufinyu wa nafasi ya kucheza mara kwa mara unaomkabili na sasa anasaka mahala ambapo atakua akipata changamoto mpya.

Tayari uongozi wa Real Madrid umeshatangaza ada ya usajili kwa ajili ya mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 22, kuwa ni pauni million 21.1.

Arsenal imetajwa kuwa mstari wa mbele katika harakati za kumuwania Jese, na kama itakua hivyo huenda klabu hiyo ikanufaika kuwa na mshambuliaji ambaye atakua mbadala wa waliopo kikosini kwa sasa, ambao mara kadhaa wanasumbuliwa na majeraha.

Jese tayari ameshaifungia Real Madrid mabao mawili katika msimu huu wa ligi, na changamoto anazokutana nazo kikosini, ni uwepo wa mchezaji kama Cristiano Ronaldo, Gareth Bale, Karim Benzema pamoja na James Rodrigues.

Jose Mourinho Huenda Akanusurika
Lowassa Kutoa Ya Moyoni Jumamosi Hii