Mapigano yameanza kati ya Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na kikundi cha M23 mara baada ya watu wengi kukimbia maeneo yanayodhibitiwa na waasi kushambuliwa na ndege za Jeshi

Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, wakaazi wameliambia shirika hilo kwamba walisikia sauti za mapigano zaidi kufikia jioni, baada ya kimya cha siku nzima.

Maafisa walisema kwamba jeshi la DRC lilitumia ndege kushambulia maeneo ya M23 mashariki mwa nchi, huku baadhi ya wakaazi wakikimbilia nje ya mpaka.

Wakati mapigano yakipamba moto, mji wa Rugari unadhaniwa kuwa karibu na msitari wa mbele wa mapambano, kilomita 30 kutoka mji wa Goma.

Umoja wa Mataifa umesema jana kuwa watu wasiopungua 188,000 wamekimbia vijiji vyao tangu Oktoba 20, yalipoanza mashambulizi mapya ya M23, ambapo takribani watu 16,500 wamejihifadhi katika nchi jirani ya Uganda.

Ugumu wa Maisha: Vijana wafikiria upya kupata watoto
Peter Banda kuikosa Ihefu FC