Jeshi la polisi limefanya operasheni Maalumu ya ukaguzi katika maeneo yaliyokuwa maficho ya wahalifu wenye kujihusisha na matukio ya unyanganyi wa kutumia silaha na matukio yenye mlengo wa kigaidi katika Mkoa wa Kipolisi Rufiji.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma Msemaji wa Jeshi la Polisi Makao Makuu ya polisi Jijini SACP David Misime, amesema kuwa kazi kubwa imefanywa katika kipindi chote cha operesheni kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama pamoja na wananchi.

Aidha SACP Misime amesema kumekuwa na mafanikio makubwa kwenye oparesheni hiyo ya kuwakamata wahalifu pamoja na silaha nyingi zikiwemo za kivita na kupelekea hali kuwa shwari na wananchi kuendelezashughuli zao za kujileta maendeleo bila hofu.

“Baada ya operasheni hiyo kubwa na hali ya amani na usalama kurejea, jeshi la polisi liliona umuhimu wa kufanya operasheni ya ukaguzi wa maeneo yaliyokuwa yanatumiwa na wahalifu kwa kipindi hicho yakiwepo eneo la wilaya ya Kibiti kama vile Rungungu na Nyambunda,” Amesema SACP Misime.

Aidha SACP Misime amesema Jeshi la Polisi limeendelea kusisitiza umuhimu wa kila Mtanzania kufuata sheria, kanuni na taratibu za nchi na anayekwenda kinyume Jeshi la Polisi litamchukulia mwananchi huyo mwenye lengo la kuvuruga amani na utulivu.

Dkt. Mpango atoa pole familia ya Kwandikwa
Auawa kisa Pombe