Rapa Joe Budden amemvaa Nicki Minaj na mpenzi wake Meek Mill kuwa ni wapumbavu huku akichochea kuni ugomvi kati yake na Drake.

Nicki na Joe Budden

Joe Budden ameeleza kuwa Nicki ni mpumbavu kwakuwa amekuwa na uhusiano wa kimapenzi na Meek ambaye pia ni mpumbavu.

Hasira za Joe Badden zinatokana na kauli aliyowahi kuitoa Nicki kwenye wimbo wake ambayo yeye anaamini ililenga kudharau ‘podcast’ yake.

“Nicki alisikika kama mpumbavu kweli. Na najua ni mpumbavu kwa sababu anapenda kuwa na wanaume wapumbavu. Kwa sababu Meek ni mpumbavu,” alisema Joe Badden.

Pia, alimuonya Drake kwa kile kilichosikika kuwa huenda akamchana kwenye wimbo wake ujao ambao atamshirikisha French Montana. Alisema akifanya hivyo itakuwa kama amerudisha beef lao la zamani na hatamvumilia.

Linah: Namzimia Sana Wizkid, Nikikuonesha Meseji hutoamini
Video: 'Mheshimiwa Mpango Usitupeleke Huko, Hatuwezi Kukubali' - Mbunge Kangi Lugola