Linah Sanga ameweka wazi jinsi anavyomzimia msanii wa Nigeria ambaye hivi sasa anapewa nafasi ya kuwa msanii anayefunika zaidi kimataifa kutoka Afrika, Wizkid Ayo.

Wizkid

Wizkid

Mkali huyo wa ‘Ole Themba’ ameiambia The Playlist ya 100.5 Times Fm kuwa amekuwa anavutiwa na Wizkid kumuziki ‘nakadhalika’.

Amesema kuwa mbali na mambo mengine, yuko katika mpango wa kufanya naye wimbo. Linah aliweka wazi kuwa amekuwa akichat na muimbaji huyo na wamekuwa watu wa karibu.

“Mimi pia nina namba zake tunachat,” alisema Linah baada ya mtangazaji wa kipindi hicho, Omary ‘Lil Ommy’ Tambwe kumwambia kuwa anaweza kumpa namba za Wizkid kama anamzimia.

“Naweza kukuonesha hapa message zetu hutoamini. Sema watu mapovu yanawatokwaa sana…,” Linah aliongeza.

Katika hatua nyingine, Mwimbaji huyo aliwaweka mguu sawa mashabiki wake kuwa baada tu ya mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ataachia wimbo wake mpya aliomshirikisha Barakah Da Prince.

 

 

 

Video: Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ amedaiwa kuonyesha alama ya dole bungeni, Naibu spika ametoa mwongozo
Joe Budden: Nicki Minaj, Meek Mill ni Wapumbavu