Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemteua, Adolf Hyasinth Mohondera Ndunguru kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango anayeshughulikia Sera.

Ndunguru ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, anayeshughulikia sera nafasi ambayo ilikuwa wazi.

Aidha, kabla ya uteuzi huo Ndunguru alikuwa Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Kufuatia uteuzi huo, Rais Magufuli amemteua, Lameck Msafiri Mbibo kuwa Naibu Kamishna Mkuu wa TRA, ambapo kabla ya uteuzi huo alikuwa meneja wa TRA mkoa Kilimanjaro.

TMA yatoa tahadhari kuhusu mvua
Waziri wa Nishati apiga marufuku mgao wa Umeme