Serikali imepanga na itahakikisha Wakazi wa Mkoa wa Katavi wanaanza kutumia umeme wa Gridi ya Taifa ifikapo mwezi june mwakani hari ambayo itawafanya Wakazi wa Mkoa huo kuwa na umeme wa uhakika na kuacha kutumia genereta za mafuta zinazoigharimu Serikali pesa nyingi kuliko mapato yanayokusanywa.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nishati, Dkt. Medadi Kaleman wakati alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Wilaya za Mpanda na Tanganyika wakati alipokuwa akizundua na kuwasha umeme wa Rea awamu ya tatu katika Vijiji vya Mchakamchaka na Ifukutwa katika Wilaya ya Tanganyika pamoja na kijiji cha Kapalala Wilayani Mpanda.

Amesema kuwa ili mkoa huo kuwa na uhakika wa umeme wa uhakikika Serikali imeanzisha mradi wa kupeleka umeme mkubwa Mkoani Katavi wa gridi ya Taifa kutoka Mkoani Tabora hadi  Mkoani Katavi hari ambayo itaufanya Mkoa huo kuwa na umeme wa uhakika .

Pia shughuli za kusafirisha umeme huo wa gridi ya Taifa imeanzia Mkoani Tabora na hadi kufikia Juni mwaka 2020 wakazi wa Mkoa wa Katavi watakuwa wameanza kutumia umeme wa gridi ya Taifa na umeme huo utakuwa umeondoa adha ya kutumia mafuta ambayo yamekuwa yakisababishia Serikali kutumia gharama kubwa .

Aidha, amesisitiza kuwa kwasasa upo umeme wa kutosha hapa nchini hivyo amepiga marufuku kuwatangazia wananchi kuwa kuna mgao wa umeme pasipo kuwa na sababu bali sehemu ambayo kuna kuwa na matengenezo ya umeme ndio sehemu hiyo pekee inayotakiwa kuwa na mgao wa umeme.

Kwa upande wake Mkuu wa  Mkoa wa  Katavi, Amos  Makalla amesema kuwa Mkoa wa Katavi ulikuwa unatumia Megawati 2.5 za umeme lakini baada ya Tanesco kuongeza genereta Mkoa huo  una umeme wa Megawati 3.7 hivyo bado wanao umeme wa ziada.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Salehe Mhando ameishukuru Serikali ya awamu ya tano kwa kuweza kufikisha umeme kwenye vijiji na vitongoji vya Wilaya hiyo ambavyo toka nchi imepata uhuru vilikuwa havija pata umeme.

JPM afanya uteuzi wa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha
Kangi Lugola awatangazia kiama matrafiki wala rushwa