Kaimu Mkurugenzi wa Mashindano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Martin Chacha amejiuzulu nafasi yake katika utumishi wa TFF kuanzia leo tarehe 5 Aprili 2016.

 Katika barua yake aliyomwandikia Katibu Mkuu wa TFF, Chacha alieleza kuwa amepata majukumu mapya ya kikazi ambayo pamoja na majukumu ya kifamilia

yatamfanya akose muda wa kutumika vema katika nafasi yake katika Shirikisho

Martin alijiunga na TFF Julai 2014 akiwa Afisa wa Mashindano na baadaye kuteuliwa kukaimu nafasi ya Mkurugenzi wa Mashindano, kufuatia aliyekuwa anashikiria nafasi hiyo Boniface Wambura kuteuliwa kuwa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB).

TFF inamtakia kila la kheri na mafanikio mema Chacha katika majukumu yake mapya.

Serikali yaweka wazi Mshahara wa Kikwete alipokuwa Rais
Mahakama ya ICC yafuta kesi dhidi ya makamu wa rais wa Kenya na Mwandishi