Malinda Lango chaguo la pili kwenye kikosi cha Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC , Beno Kakolanya leo Alhamisi (Agosti 19) amepoteza mama yake mzazi anayeitwa Eva Mwankusye na msiba upo kwao Isyesye jijini Mbeya.

Taarifa za msiba huo zimethibitishwa na kaka wa mchezaji huyo, Asajile Mwakalindile ambaye alikuwa na mama huyo muda wote huko jijini Mbeya.

Mwakalindile amesema: “Ni kweli mama amefariki leo asubuhi na bado tupo hospitali.”

Kakolanya yupo nchini Morocco na kikosi cha Simba SC katika maandalizi ya msimu mpya, lakini taarifa kutoka kwenye kambi ya Mabingwa hao zinaeleza kuwa, Mlinda Lango huyo ataanza safari ya kurejea nyumbani kesho Ijumaa (Agosti 20), kwa ajili ya mazishi ya mama yake.

Simba SC imeweka kambi nchini Morocco, kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara na Michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika itakayoanza mwezi Septemba.

Fiston: Young Africans imekosea sana
Yusuph Muhilu: Kagera Sugar walijua kila kitu