Kero ya ukosefu wa maji safi na salama kwa wananchi wengi nchini inatarajiwa kupungua kwa kasi ifikapo mwezi Juni mwakani baada ya serikali ya awamu ya tano kuazimia kuwaunganishia maji safi wateja wapya milioni 1.

Hayo yamebainishwa hivi karibuni na waziri wa maji na umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa, alipokuwa akikagua mitambo ya maji ya Ruvu Juu na Ruvu Chini ikiwa ni mara ya kwanza tangu alipoapishwa.

Profesa Mbarawa alisema kuwa serikali imeazimia kuwaunganisha kwenye mfumo rasmi wa maji safi na salama wateja hao ikiwa ni pamoja na kuhakikisha mabomba maarufu kwa jina la ‘Mabomba ya Mchina’yaliyopita katika maeneo ya jiji la Dar es Salaam yanaanza kutoa maji.

“Ujenzi wa miundombinu hii ya maji inayotoka Ruvu Juu hadi kufika Dar es Salaam unaenda vizuri na tunategemea kabisa inapofikia mwezi Februari mwakani kazi hii inamalizika,” alisema profesa Mbarawa.

Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASCO, Cyprian Luhemeja alimueleza Waziri wa Maji na Umwagiliaji kuwa mradi huo ulicheleweshwa kwa kuwa wananchi waliokuwa katika maeneo ambayo mradi huo unapitia waliipeleka serikali mahakamani.

TP Mazembe Yaambulia Nafasi Ya Sita Duniani
Ashinda Udiwani Kwa Tiketi ya Chadema akiwa gerezani