Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Dk. John Magufuli imepanga kuwaondolewa mzigo wa kodi watu wanaopanga katika nyumba mbalimbali na kuweka viwango vya kodi kulingana na hadhi ya nyumba husika.

Hayo yalisema jana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi alipokuwa akitoa ufafanuzi kuhusu utaratibu wa kupangisha nyumba pamoja na ujenzi wa nyumba ‘za bei nafuu’ unaofanywa na mashirika mbalimbali ya umma ikiwemo NHIF, NHC, PPF na NSSF.

Waziri Lukuvi alisema kuwa wenye nyumba wamekuwa wakiwapangia wapangaji bei wanayotaka wao na kwamba nyumba nyingi hazina hadhi ya bei husika inayolipwa. Alisema kuwa Serikali itapanga bei elekezi za nyumba za kupangisha kulingana na hadhi na huduma inayopatikana katika nyumba husika.

Katika hatua nyingine, Lukuvi alikosoa ujenzi wa nyumba zinazoitwa ‘za bei nafuu’ unaofanywa na mashirika mbalimbali ya umma nchini akieleza kuwa hakuna shirika hata moja hivi sasa lililojenga nyumba inayoweza kufikia kiwango cha kuitwa ya ‘bei nafuu’.

“Hizo nyumba zote zilizojengwa na mashirika, hakuna hata moja ambayo inakidhi kigezo cha kuitwa ya bei nafuu, hakuna hata shirika moja ambalo limejenga nyumba ya bei nafuu hadi sasa,” alisema.

Serikali kuifumua Dar na kuipanga upya
Bunge laja kivingine, Vyombo vya habari kupata matangazo yake bila kufunga mitambo Bungeni