Serikali imeazimia kulifumua na kulipanga upya jiji la Dar es Salaam baaa ya kukamilika kwa mpango mpya kuanzia mwezi Julai mwaka huu.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Mkazi, William Lukuvi amesema kuwa jiji hilo litafumuliwa na kupangwa upya ndani ya kipindi cha miaka 10 ili liwe jiji la kisasa na kwamba hivi sasa jiji hilo linaongoza kwa mpango mbovu wa miji.

Waziri Lukuvi aliyasema hayo jana alipokuwa akizungumza na wadau wa Sekta ya Uendelezaji Ujenzi jijini Dar es Salaam. Alisema kuwa awali, Serikali ilimpa kazi Mshauri wa Mpango Miji kutoka Italia akishirikiana na wataalam wa ndani lakini mshauri huyo ameonekana kushindwa kazi licha ya kulipwa fedha.

Fahamu sakata la Helikopita ya Polisi kutumwa Pochi ya Gavana Nyumbani kwake
Kasi ya Magufuli kuwayoosha wenye nyumba za kupangisha