Uongozi wa Azam FC umeeleza kwamba unatamani kulitwaa Kombe la Mapinduzi ili kuwaongezea hamasa wachezaji wao kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kauli hiyo imetolewa na Mtendaji Mkuu wa timu hiyo, Saad Kawemba wakati akizungumza na badhi ya vyombo vya habari hivi karibuni. Alisema, kikosi chao kimeendelea kufanya vyema kutokana na kuwepo ushirikiano mkubwa ndani ya timu hiyo kwa viongozi pamoja na wachezaji.

“Bado tunaangalia wapi tutakwenda kuweka kambi baada ya michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika ili tuweze kufanya vizuri mwaka huu,” alisema.

De Bruyne Afichua Siri Ya Kuachana Na Chelsea
Mwigulu Nchemba asimamisha watumishi wengine na kuvunja bodi