Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba leo amefanya ziara katika machinjio yaliyoko Mkoani Pwani na kuwasimimisha baadhi ya watumishi kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za umma.

Kadhalika, Waziri Nchemba ameagiza kusimamishwa malipo ya mshauri wa ujenzi wa machinjio ya kisasa yaliyopo Ruvu mkoani humo.

Katika hatua nyingine, Nchemba ameamuru kuvunjwa kwa bodi iliyokuwa ikisimamia ujenzi wa machinjio hayo kwa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha. Ameagiza bodi hiyo kukoma rasmi kesho kutwa (Januari 6, 2016).

 

Kawemba: Tuna Uchu Na Ubingwa Wa Mapinduzi
Guardiola: Sijajua Ninakwenda Wapi ...