Leo June 11, 2018 Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Wilbard Mashauri ametupilia mbali pingamizi la viongozi wa Chadema akiwemo Freeman Mbowe la kutaka kesi ya kufanya maandamano ifutwe badala yake ameagiza hati ya mashtaka ya kesi hiyo ifanyiwe marekebisho.
Ambapo Mashauri amesema amekubaliana na hoja 2 za upande wa mashtaka kati ya hoja 8 ambazo ziliwakilishwa Mahakamani na upande wa mashtaka.
Hata hivyo, upande wa utetezi kupitia wakili wao, Peter Kibatala umetangaza nia ya kutoridhia na maamuzi hayo yaliyotolewa na Hakimu na kudai kukata rufaa kupinga uamuzi huo.
Wakili wa serikali Mkuu, Paul Kadushi umedai kuwa kwa mujibu wa Sheria ya Mahakama za Mahakimu hakuna uwezekano wa kukata rufaa katika uamuzi mdogo ambao hauwezi kuathiri kesi.
-
TCRA yapiga ‘stop’ mitandao isiyojisajili kuhabarisha, Jamii Forum yatii amri
-
Serikali kuchakachua sheria ya Uzazi na Afya, wanaume nao watajwa kunufaika
“Naomba mahakama ipuuzie hoja hizo na nia hiyo ni batili,”ameeleza Kadushi.
Aidha uamuzi juu ya rufaa ya kesi hiyo umetangazwa kutolewa June 12, 2018 na Hakimu Mkazi Mashauri baada ya mvutano mkali kati ya pande hizo mbili.
Washtakiwa wa kesi hiyo ni viongozi wa nyadhifa kubwa katika chama cha upinzani Chadema akiwemo, Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe, Mbunge wa Mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalimu na Naibu katibu Mkuu bara na Mbunge wa kibamba John Mnyika, Mbunge wa Tarime mjini Esterher Matiko, Katibu wa chama hicho Dk Vicenti Mashinji, Mbunge wa Kawe Halima Mdee, mbunge wa Tarime vijijini, John Heche na mbunge wa Bunda, Ester Bulaya.
Washtakiwa hao wanakabiliwa na jumla ya mashtaka 12 katika kesi ya jinai namba 112 ya mwaka 2018 ikiwamo kula njama, kufanya mkusanyiko usio halali kinyume cha sheria na kuendelea kufanya mkusanyiko usio halali ama maandamano yaliyosababisha kifo cha Akwilina.