Mtoto mchanga wa kike ameokotwa na msamalia mwema akiwa amefungwa ndani ya box la kuuzia viatu baada ya kutelekezwa kichakani katika eneo la Guangdong nchini China.

Kwa mujibu wa kipande cha video kinachoonesha sehemu ya tukio hilo, ‘Msamalia’ huyo aligundua box hilo lenye mtoto alipopita karibu na eneo hilo. Mwanamke huyo alidai kuwa alipofungua box alimuona kichanga akiwa ametapakaa damu, hali inayoashiria kuwa alikuwa amezaliwa saa chache zilizopita.

Alieleza kuwa alimkimbiza haraka katika hospitali ya watoto iliyokuwa karibu zaidi. Kwa mujibu wa Daily Mail, baada ya kufanyiwa vipimo mtoto huyo alionekana kuwa katika hali nzuri kiafya.

“Anaonekana kuwa na hali nzuri kwa sababu sasa hivi sioni kitu chochote kisicho cha kawaida kwake,” Daktari anasikika kwenye sehemu ya video ya tukio hilo.

Hata hivyo, haijajulikana idadi ya saa ambazo mtoto huyo alikaa ndani ya box hilo la viatu.

Ulishangaa ya kichanga Tiffah wa Diamond? Utastaajabu ya mapacha wa Jay Z
Magazeti ya Tanzania leo Julai 21, 2017