Zanzibar Heroes imeifunga Kilimanjaro Stars mabao 2-1 katika mchezo wake wa pili wa hatua ya makundi ya michuano ya Kombe la Chalenji inayoendelea nchini Kenya.

Katika mchezo huo wa Kundi A, uliopigwa kwenye Uwanja wa Kenyatta uliopo Machakos, Kenya, Kilimanjaro Stars ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 28 kupitia kwa nahodha wake, Himid Mao.

Zanzibar Heroes ilisawazisha bao hilo dakika ya 66 kupitia kwa Kassim Khamis, kabla ya Ibrahim Ahmada kuongeza la pili na la ushindi dakika ya 78.

Kilimanjaro Stars ilipata pigo katika dakika ya nne baada ya beki wake, Kelvin Yondani kuumia na kushindwa kuendelea na mchezo huo, huku nafasi yake ikichukuliwa na Boniface Maganga.

Kwa ushindi huo, Zanzibar Heroes imefikisha pointi sita baada ya kushinda mechi zake zote mbili, huku Kilimanjaro Stars ikiwa na pointi moja kutokana na kutoka sare moja na kupoteza moja.

Bado tuna nafasi - Ninje
Majaliwa: Rais Magufuli kuhamia Dodoma mwakani