Msanii wa muziki wa kizazi kipya Ali Killy, maarufu kama Killy, kutoka katika kundi la muziki la Konde Gang ameikumbuka lebo yake ya zamani Kings Music Records kwa kusema hajafuta na hawezi kufuta namba za wasanii aliowaacha kwenye lebo hiyo kwani bado ni familia yake.

Amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kujibu tetesi ambazo zinadai kuwa amefuta namba za wasanii wa Kings Music Records na hawana mawasiliano tena baada ya kusainiwa Konde Gang ya Harmonize.

“Konde Gang wamenipokea kwa mikoni miwili, kuna upendo sana na tunaishi kifamilia kabla ya kazi, sijafuta namba ya mtu yeyote kila kitu kipo vilevile wale bado ni ndugu zangu na hatujagombana sijaongea na Alikiba ila Abdukiba nazungumza naye” amesema Killy 

Killy na Cheed walitangaza kujitoa Kings Music Records ya Alikiba siku ya Aprili 14, 2020 ambapo kwa sasa wapo lebo ya Konde Gang chini ya msanii Harmonize.

Kaze: Ninawaamini Sogne, Sarpong
Azam FC yatua Mbeya, kuikabili Ihefu FC kesho

Comments

comments