Rapper John Simon maarufu kama Joh Makini ameitambulisha lebo yake ya muziki iitwayo ‘Makini Records’ pamoja na kumtambulisha msanii mpya Ptuck William ndani ya lebo hiyo.

Joh Makini ambaye anawakilisha kundi la Weusi amesema amekuja na lebo hiyo ili kusaidia vipaji vipya viweze kujulikana kwenye kiwanda cha muziki wa Bongo.

Amesema kwa muda mrefu alikuwa anatamani kufanya hivyo lakini alikuwa anashindwa kutokana na mtaji wa kuwekeza ambapo kwa sasa amesema yupo tayari kuwasaidia wasanii wenye vipaji.

Joh amewataka mashabiki wake kuisapoti lebo hiyo ili kusaidia vipaji vya wasanii wa Bongo na kukuza muziki wa Bongo Fleva pamoja na muziki wa Hip Hop.

“Makini Records” tayari ina mwanamuziki mmoja aliyetambulishwa leo(jana), na ameshaachia kazi yake ya kwanza akiwa na Joh Makini, ngoma inaitwa “Mbele kwa Mbele”.

"Corona isiwe kisingizio, mradi ukamilike kabla ya Novemba" - Rais Magufuli
Magufuli: Kunenge nataka ubadilike

Comments

comments