Rais wa Chama cha Soka nchini Ufaransa (FFF), Noel Le Graet amedokeza kwamba angependelea nahodha wa timu ya Taifa ya Ufaransa, Hugo Lloris asivae kitambaa cha LGBT katika Fainali za za Kombe la Dunia nchini QATAR.

Le Graet amesisitiza kwamba wanapaswa kuonyesha heshima kwa nchi mwenyeji (QATAR), ambao wanapiga vikali mahusiano ya jinsi moja na hata wale wanaofanya mapenzi wawe wanandoa kinyume na hapo sheria itachukua mkondo wake.

Nahodha Hugo Lloris anaonekana kukubaliana dokezo hilo la Rais wa FFF, Le Graët na kusema kwamba: “Kwanza, kabla ya kufanya lolote tunahitaji FIFA na FFF kukubaliana nalo. Kwa kweli, nina maoni yangu ya kibinafsi, na yanalingana na ya rais.”

“Tunapokaribisha wageni mara nyingi tunawataka wafate sheria zetu na kuheshimu utamaduni wetu na nitafanya vivyo hivyo nitakapoenda Qatar sina budi kuonyesha heshima kuhusiana na hilo.”

Katika Fainali za Kombe la Dunia mwaka huu, Ufaransa Imepangwa Kundi D na itaanza Kampeni ya kutetea Ubingwa wake dhidi ya Australia Novemba 22, katika Uwanja wa Al Janoub, mjini Al Wakrah.

Mchezo wa pili itapapatuana na Denmark Novemba 26 kwenye Uwanja wa 974, mjini Doha na Novemba 30 itamaliza hatua ya Makundi kwa kuikabili Tunisia mjini Al Rayyan katika Uwanja wa Education City.

Tunisia yapata mapokezi makubwa QATAR
Majaji wapitisha sheria mpya ya kuchapa, kukata mkono