Timu ya Taifa ya Tunisia imepata mapokezi makubwa ilipowasili katika mji mkuu wa Qatar, Doha tayari kwa Fainali za Kombe la Dunia zinazotarajiwa kuanzia Jumapili (Novemba 20).

Tunisia ambayo imepangwa kundi D pamoja na mabingwa watetezi Ufaransa, Australia na Denmark iliwasili usiku wa kuamkia leo Jumanne (Novemba 15) nchini humo.

Watunisia wengi wanaoishi Mashariki ya Kati pamoja na mashabiki waliosafiri, wamejitokeza kuilaki timu yao ya Taifa huku wakiwa na matumani itafanya vizuri.

Tunisia ni miongoni mwa Mataifa matano ya Afrika yanayowakilisha Bara hilo kwenye Fainali za Kombe la Dunia mwaka huu 2022.

Nchi nyingine kutoka Afrika ni Ghana, Morocco, Cameroon na Senegal.

Kikosi cha Tunisia kilichotajwa tayari kwa Fainali hizo upande wa Walinda Lango ni: Aymen Dahmen, Bechir Ben Said, Aymen Mathlouthi, Mouez Hassen

Mabeki: Wajdi Kechrida, Mohamed Drager, Dylan Bronn, Nader Ghandri, Bilel Ifa, Yassine Meriah, Montassar Talbi, Ali Maaloul, Ali Abdi

Viungo: Ghailene Chaalali, Aissa Laidouni, Eliyes Skhiri, Hannibal Mejbri, Ferjani Sassi, Mohamed Ali Ben Romdhane

Washambuliaji: Wahbi Khazri, Youssef Msakni, Taha Yessine Khenissi, Issam Jebali, Seiffedine Jaziri, Anis Ben Slimane, Naim Sliti

Tunisia itaanza Kampeni ya kusaka ubingwa wa Dunia mwaka huu, Novemba 22 kwa kucheza dhidi ya Denmark mjini Al Rayyan katika Uwanja wa Education City.

Novemba 26 wababe hao kutoka Afrika Kaskazini watarejea tena Dimbani kupapatuana na Australia mjini Al Wakrah kwenye Uwanja wa Al Janoub, na mchezo wa mwisho hatua ya Makundi watacheza dhidi ya Mabingwa watetezi Ufaransa mjini Al Rayyan, katika Uwanja wa Education City, Novemba 30.

Mashabiki kulindwa na teknolojia QATAR
Kitambaa cha LGBT chaibua mzozo Ufaransa