Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) leo imebaini uwepo wa kiwanda cha kuzalisha vipodozi na manukato ‘bandia’ kilichoko eneo la Kigamboni Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Hiiti Sillo amesema kuwa wamefanikiwa kubaini uwepo wa kiwanda hicho baada ya kupewa taarifa na wasamalia wema.

Amesema kuwa taarifa hizo zilizowawezesha pia kukamata moja kati ya maduka ya vipodozi hivyo bandia kutoka kiwandani humo, linalomilikiwa na Dk. Mohammed Gwao, katika eneo la Sinza Kijiweni jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa TFDA amesema kuwa walifanikiwa kukamata jumla ya chupa 5350 za manukato hayo bandia zenye thamani ya shilingi milioni 107 zinazozalishwa na kiwanda hicho na kuwekewa nembo inayoonesha kuwa yamezalishwa nje ya nchi.

Baada ya kumhoji Dk. Gwao anayemiliki duka lililokutwa na vipodozi hivyo bandia, alisisitiza kuwa bidhaa hizo ameziingiza nchini kutoka nchini Uturuki kupitia Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.

Hata hivyo, TFDA ilipomtaka atoe vielelezo vya uingizaji bidhaa hizo alishindwa kuvionesha.

Cheka aomba Magufuli ajivunie ushindi wake
Serikali yalitaka gazeti la 'Dira ya Mtanzania' kumuomba radhi Sefue kwa kumuita 'jipu'