Mchezaji mashuhuri wa mpira wa vikapu nchini Marekani, Kobe Bryant usiku wa kuamkia hii leo alicheza mchezo wake wa mwisho, akiwa na klabu yake ya Los Angeles.

Hatua hiyo imedhihirisha rasmi Kobe amefunga ukurasa wa kihistoria wa miaka 20 kucheza katika ligi ya NBA kwa kishindo.

Bryant mwenye umri wa miaka 37 alipachika pointi 60 ikiwa ni nyingi zaidi katika msimu huu na kuipatia timu yake ya Lakers ushindi wa point 101 dhidi ya 96 za wageni wao Utha Jazz, mbele ya maelfu ya mashabiki waliokua wamefurika kwenye uwanja wa Staples Center na mamilioni ya watazamaji na mashabiki kote duniani.

Bryant aliyejulikana kama “The Black Mamba” alichezea Lakers kwa miaka 20 na kua mchezaji aliyebaki katika timu moja kwa muda mrefu zaidi katika historia ya ligi ya mpira wa kikapu nchini Marekani NBA.

Matukiko mengine ya kihistoria yaliyofanywa na Kobe Bryant wakati akicheza mpira wa kikapu kabla ya kustaafu usiku wa kuamkia hii leo ni kunyakua taji la mabingwa wa NBA mara tano, mara tatu ikiwa ni mfululizo kati ya mwaka 2000 – 2001, akitajwa mchezaji bora wa michuano ya fainali mara mbili mfululizo.

Anakua mchezaji wa tatu wa NBA kupachika pointi nyingi akiwa nafasi moja na bingwa Michael Johnson.

Kwa ujumla amepachika pointi 33,643, ambapo katika michuano 25 amepata zaidi ya pointi 50, ikiwa ni pamoja na mchezo wake wa mwisho wa usiku wa kuamkia hii leo.

TUNAMTAKIA KILA LA KHERI KOBE BRYANT “THE BLACK MAMBA” KATIKA MAISHA YAKE YA NJE YA UWANJA WA MPIRA WA KIKAPU. INSHAALLAH

Golden State Warriors Wavunja Rekodi Ya Chicago Bulls
Ravia, Ali Mohammed Na Zam Ally Wakabidhiwa Soka La Zanzibar